Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kutimiza ahadi ya kugawa chakula (mahindi) bure kwa wananchi waliohama kwa hiari kutoka Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Kijiji cha Msomera mkoani Tanga
Dhumuni la kugawa mahindi hayo kwa wananchi kila baada ya miezi mitatu ni utekelezaji wa ahadi ya Serikali kutoa chakula bure kwa wananchi hao kwa muda wa miezi 18 wakati wakiendelea kuzoea mazingira mapya waliyohamia kabla ya kulima na kuvuna kupitia mashamba waliyopewa na Serikali.
Katika mgao wa mwezi Oktoba, jumla ya magunia 1,058 yenye tani 95.22 yamegawanywa kwa Kaya 529 ambapo baada ya mgao huo wananchi hao wameendelea kuishukuru serikali kwa kuendelea kuwajali katika huduma ya chakula na kuendelea kuboresha huduma za kijamii ikiwemo vituo vya afya, shule, maji, umeme, barabara, mawasiliano, posta, majosho na malambo.