[caption id="attachment_11300" align="aligncenter" width="896"] Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Mhandisi Stella Manyanya akifurahia jambo na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Wasichana ya Tabora jana alipokwenda kukagua shughuli za ukarabati wa majengo unaoendelea. (Picha na Tiganya Vincent-RS Tabora.)[/caption]
Na: Tiganya Vincent, RS-TABORA
SERIKALI imewaonya wanafunzi kuepuka matumizi ya dawa za kulevya ambayo ndio wakati mwingine yawasababisha kujiingiza katika vitendo vya uhalifu na vurugu ambazo hatimaye zinawasababisha baadhi yao kusimamishwa masomo na kukatiza ndoto zao.
Agizo hilo limetolewa jana wilayani Tabora na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Mhandisi Stella Manyanya wakati alipotembelea Shule ya Sekondari ya Tabora ili kujionea maendeleo ya ukarabati chini ya utaratibu wa ukarabati wa Shule Kongwe hapa nchini.
Aliwaambia kuwa wanafunzi wote nchini wanatakiwa kufuata Sheria za Shule na za Nchi ili kuhakikisha anamaliza masomo yake bila kupata matatizo ikiwemo kufikishwa mahakamani.
“Unatakiwa kufuata Sheria na taratibu za shule kama ulivyoelekeza , ukitoroka shule na kwenda mitaani ukileta fujo …ukileta vurugu utashughulikiwa kama ulivyokutwa huko huko…kwa sababu mwanafunzi anatakiwa kuwa eneo la shule sawa “ alisisitiza Naibu Waziri huyo.
Akitoa taarifa ya ukarabati unaoendelea Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Tabora Marwa Robert alisema kuwa hadi hivi sasa kazi mbalimbali zimekwisha fanyika
Hivi karibuni Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Milambo walitoroka shuleni usiku na kuvamia sherehe za mkazi wa Tabora