[caption id="attachment_42760" align="aligncenter" width="800"] Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt Hassan Abbas akisisitiza jambo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika leo Jijini Dodoma.Kulia kwake ni Balozi wa Uingereza Nchini Bi.Sarah Cooke na Kaimu Balozi wa Marekani Nchini Bi.Inmi Patterson na Kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri(TEF) na Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari nchini bw.Kajubi Mukajanga .[/caption]
Na Immaculate Makilika –MAELEZO
Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imesema kuwa imependekeza kuuundwa kwa Kamati Maaluum ya Kitaifa itakayowashirikisha wanahabari ili kujadili changamoto na kutafuta suluhu ili katika sekta ya habari.
Akizungumza leo jijini Dodoma katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, yaliyofanyika jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, kwa niaba ya mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, amesema kuwa Serikali imedhamiria kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya habari nchini kwa kufanya majadiliano ya pamoja na wadau wa wahabari
[caption id="attachment_42758" align="aligncenter" width="800"] Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt Hassan Abbas akipokea zawadi ya mfuko kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini (UTPC) Bw.Aboubakar Karsan wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika leo Jijini Dodoma.[/caption]Dkt. Abbasi amesema: “Tutaunda kamati ya kitaifa ya wataalamu kati ya Serikali na wanahabari kuangalia changamoto za kisera, kisheria na kisiasa zilizopo katika sekta ya habari nchini. Kamati hii itakuja na suluhu ya masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutatua kero ya wanahabari”
Ameeleza kuwa pendekezo hilo la Serikali ambalo lilikubaliwa katika mkutano huo, litafungua ukurasa mpya katika sekta ya habari ambapo Kamati itaangalia kwa upana zaidi mandeleo ya sekta ya habari na si malalamiko yanayotolewa na wanahabari pekee kuhusu Sheria yaHuduma za Habari kwa kudai kuwa ni kandamizi.
[caption id="attachment_42756" align="aligncenter" width="800"] Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt Hassan Abbas(mwenye suti ya Bluu) akitazama kazi za uandishi wa habari wakati akitembelea mabanda mbalimbali wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika leo Jijini Dodoma.[/caption]Dkt. Abbasi alifafanua kuwa baadhi ya mikanganyiko inatokana na baadhi ya waandishi wa habari kutokuwa na uelewa wa Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 ambapo wanadai ni Sheria kandamizi lakini hawataji hata aina ya vifungu. Amesema kuwa Sheria hiyo sio mbaya na kutolea mfano wa Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 ambayo ilimpa mamlaka makubwa Waziri wa Habari ya kufungia gazeti bila hatua nyingi kama ilivyo hivi sasa.
[caption id="attachment_42762" align="aligncenter" width="800"] Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt Hassan Abbas akizungumza na wanafunzi kutoka Chuo cha mafunzo ya Uandishi wa Habari Dodoma (Dodoma Media College) wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika leo Jijini Dodoma.[/caption]Aidha, Dkt Abbasi alisema kuwa Serikali inaheshimu na kuelewa umuhimu wa sekta ya habari nchini na hivyo itaendelea kushirikiana na sekta hiyo ikiwa ni sambamba na kuendelea kutoa usajili kwa magazeti ili watanzania waweze kupata sauti tofauti ikiwa ni pamoja na kufikiwa hadi katika maeneo ya vijijini.
Kuhusu jitihada za Serikali katika kutoa uhuru wa vyombo vya habari nchini pamoja na haki ya kupata taarifa Dkt. Abbas amesema kuwa Serikali ilitunga Sheria ya Haki ya kupata Taarifa ya mwaka 2016 ili kumsaidia mwanahabari kukusanya, kuchakata na kusambaza habari.
Jitihada nyingine ni pamoja na kuwawajibisha Maafisa wa Serikali ambao wameonekana kutotimiza matakwa ya Sheria hiyo kwa kutotoa taarifa kwa umma na kwa wakati.
Kwa upande wake, Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Sarah Cooke alisema kuwa Serikali yake itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika masuala ya sekta ya habari, ambapo Serikali ya Uingereza itatoa shilingi bilioni 7.8 kwa ajili ya mafunzo kwa wanahabari.
Naye, Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Imn Peterson alisema kuwa hakuna diplomasia iliyokamilika bila upatikanaji wa habari za wazi na kuaminika na ni nguzo ya kujenga taasisi za haki na zisizo na upendeleo.
Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwa siku mbili nchini, yamefikia kilele leo Mei 2, 2019 ambapo kimataifa yamefanyika Adis Ababa nchini Ethiopia.