[caption id="attachment_29470" align="aligncenter" width="891"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumzia mikakati ya Serikali kupambana na janga la Ukimwi hapa nchini wakati wa warsha kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya mapema leo Bungeni mjini Dodoma. kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira Mhe. Antony Mavunde.
Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma
Serikali imesema itaendeleza mapambano ya Vita dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi kwa kuongeza kasi katika kuzuia maambukizi mapya ikiwemo kutoa elimu kwa umma.
Akizungumza leo mjini Dodoma wakati wa warsha kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshugulikia Ukimwi na Madawa yakulevya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa dhamira ya Serikali baada ya kuanzisha mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) ni kuhakikisha kuwa mfuko huo unajengewa uwezo ili lengo la kuanzishwa kwake litimie.
[caption id="attachment_29472" align="aligncenter" width="884"] Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibi Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Leonard Maboko akiwasilisha mada kuhusu hali ya Ukimwi hapa nchini wakati wa warsha kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya mapema leo Bungeni mjini Dodoma."Tayari mfuko umeweza kukusanya bilioni 279 katika kipindi kilichopita na mwaka huu bilioni 3 zimetengwa katika Bajeti na zitaingizwa katika mfuko huu ili uweze kutimiza majukumu yake kwa ufanishi na tumekuwa tukiwashirikisha wadau katika kuchangia na wamekuwa wakituunga mkono na tunaendelea kuwaomba wajitokeze zaidi kuchangia mfuko huu " Alisisitiza Mhagama.
Akifafanua Mhe. Mhagama amesema kuwa tayari mapendekezo kuhusu kuwepo kwa tozo maalum katika kodi yameshawasilishwa katika kamati husika kwa hatua zaidi dhamira ikiwa ni kuujengea mfuko huo uwezo wa kuwa na fedha za kutosha katika kufanikisha vita dhidi ya Ukimwi hapa nchini.
Mkakati mwingine ni ujenzi wa kituo maalum katika eneo la Mererani Mkoani Manyara kitakachosaidia katika mapambano dhidi ya Ukimwi kwa kuwa eneo hilo ni moja ya maeneo yenye mwingiliano mkubwa wa watu kutokana na shughuli za uchimbaji madini.
[caption id="attachment_29475" align="aligncenter" width="900"] Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibi Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Leonard Maboko (katikati) akitoka nje ya Viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma mara baada yakuwasilisha mada kuhusu hali ya ukimwi hapa nchini wakati wa warsha kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ukimwi na Madawa yakulevya mapema leo Bungeni mjini Dodoma. ( Picha zote na Frank Mvungi, Maelezo Dodoma)[/caption]Hatua nyingine ni kufanya kazi kwa kushirikiana kati ya TACAIDS na Mamlaka ya Kupambana na Dawa za Kulevya ili kuwafikia waathirika wa dawa za kulevya ambao ni moja ya makundi yanayoathika na ugonjwa wa ukimwi kwa mujibu wa tafiti mbalimbali.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Osca Mukasa (Mb) amesema kuwa kutengwa kwa fedha katika bajeti ya 2018/19 zitakazopelekwa katika mfuko wa kudhibi Ukimwi ni ishara nzuri kuwa serikali imeweka mkazo katika mapambano dhidi ya janga hilo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dkt. Leonard Maboko amesema Tume hiyo iko katika hatua za mwisho za kukamilisha mkakati wa Nne unaolenga kuongeza nguvu ili kufikiwa kwa malengo ya mkakati huo.
Akifafanua Dkt. Maboko amesema kuwa Tume hiyo imeandaa kampeni maalum kuhamasisha wananchi kupima ili kujijua kama wameambikizwa virusi vya ukimwi au laa hali itakayowasaidia kuchukua hatua stahiki na kwa wakati hivyo kuzuia maambukizi mapya hasa kwa vijana.
"Hapa nchini kwa mwaka kuna maambukizi mapya elfu 81,000 hivyo ni vyema tukaungana katika mapambano dhidi ya ugonjwa huu kwa kuwa uwezo wa kuzuia maambuki mapya tunao". Alisisitiza Dkt. Maboko.
Warsha kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya imefanyika mjini Dodoma leo ikiwashirikisha wajumbe wote wa kamati hiyo, Aidha mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) unalenga kuongeza rasilimali fedha kutoka asilimia 7 (2015) hadi asilimia 30 (2018).