Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali: Tutaendelea kuhakikisha wananchi wanazijua haki zao na kuziishi.
Dec 12, 2019
Na Msemaji Mkuu

Na Mwandishi Wetu

Serikali imesema imeendelea kuwashirikisha vijana katika masuala mbalimbali ya ujenzi wa uchumi wa nchi kwani ni muhimu kwao kushiriki kikamilifu katika suala hilo.

Hayo yamebainika katika kongamano la haki za binadamu na mipango ya maendeleo endelevu lililofanyika Jijini Dar es Salaam ambalo liliwashirikisha vijana kutoka vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini.

Akizungumza katika kongamano hilo, Makamu Mwenyekiti wa Haki za Binadamu na Utawala Bora Tanzania, Mohammed Hamisi, amesema kuwa vijana ni muhimu kujua maana na haki za binadamu ili kuwaleta pamoja katika kutekeleza mipango ya maendeleo endelevu kwa ujenzi wa taifa.

“Yote haya ni mwendelezo wa sherehe za kusherehekea siku ya haki za binadamu duniani na dhumuni la kongamano hili ni kuwaleta pamoja vijana walioko vyuoni ili kujua nini maana ya haki za binadamu na malengo ya maendeleo endelevu na kujadili pamoja masuala hayo”, Alisema Bw.Hamis.

Aidha Bw. Hamis alieleza jinsi gani kongamano hilo litawajengea vijana uelewa juu ya haki za binadamu na mipango endelevu kwa maendeleo ya nchi, huku akizitaja haki hizo kuwa ni haki za kiraia na kisiasa, haki za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni ambazo huwa zinawawezesha kuwa huru.

Aliongeza kuwa katika kuwashirikisha vijana kwenye hayo masuala mawili italeta chachu kubwa kwa wananchi kuelewa nini maana ya haki ili waweze kuziishi katika maeneo yao, kwa hiyo ushirikishwaji wao katika kongamano hilo utaleta mabadiliko vyuoni na kuwa na mwamko mkubwa wa kujua haki za binadamu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uangalizi wa Maliasili na Utajiri wa Rasilimali za Asili kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Bi. Neema Mwanga, alisema kuwa lengo la Wizara na Serikali kwa ujumla ni kuhakikisha wananchi wanazijua haki zao na kuziishi.

“Sisi kama Wizara ya Katiba na Sheria tunawajibu mkubwa wa kuhakikisha kuwa wananchi wanazijua haki zao na kuziishi, na kama kuna sheria imetungwa imeenda kinyume na haki za binadamu tunaipitia na kuirekebisha, na tumerekebisha sheria nyingi na tutaendelea kufanya hivyo ili kuendasna na haki za binadamu duniani”, Alisema Bi.Mwanga.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi