[caption id="attachment_46440" align="aligncenter" width="803"] Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Agustine Ndugai akitoa taarifa ya kuanza kutumia mfumo wa Tehama badala ya badala ya mfumo wa makaratasi katika kuwasilisha orodha ya shughuli za bunge wakati wa Mkutano wa 16 wa Bunge, Kikao cha Kwanza leo jijini Dodoma tarehe 3 Septemba 2019.[/caption] [caption id="attachment_46442" align="aligncenter" width="826"] Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Miraji Mtaturu akila kiapo mbele ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Agustine Ndugai wakati wa Mkutano wa 16 wa Bunge, Kikao cha Kwanza leo jijini Dodoma tarehe 3 Septemba 2019.[/caption] [caption id="attachment_46443" align="aligncenter" width="768"] Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Miraji Mtaturu akisalimiana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenyeulemavu, Mhe. Jenista Mhagama mara baada ya kula kiapo wakati wa Mkutano wa 16 wa Bunge, Kikao cha Kwanza leo jijini Dodoma tarehe 3 Septemba 2019. Kutoka kulia ni Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Adeladus Kilangi.[/caption] [caption id="attachment_46445" align="aligncenter" width="768"] Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe(kulia), Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako(kushoto) na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (katikati) wakifurahia jambo wakati wa Mkutano wa 16 wa Bunge, Kikao cha Kwanza leo jijini Dodoma tarehe 3 Septemba 2019.[/caption] [caption id="attachment_46446" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akijibu swali wakati wa Mkutano wa 16 wa Bunge, Kikao cha Kwanza leo jijini Dodoma tarehe 3 Septemba 2019.[/caption] [caption id="attachment_46447" align="aligncenter" width="967"] Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias Kwandikwa akifafanua jambo walipokuwa akijibu swali katika Mkutano wa 16 wa Bunge, Kikao cha Kwanza leo jijini Dodoma tarehe 3 Septemba 2019.[/caption] [caption id="attachment_46448" align="aligncenter" width="944"] Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ulinzi, Mhe. Mussa Hassan Zungu akiwasilisha Azimio la Bunge la kupmpongeza Mhe. Rasi Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa SADC na kuendesha vyema Mkutano wa 39 wa Jumuiya hiyo wakati wa Mkutano wa 16, Kikao cha Kwanza leo jijini Dodoma tarehe 3 Septemba 2019.[/caption] [caption id="attachment_46449" align="aligncenter" width="946"] Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Boniphace Simbachawene (aliyesimama) akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Bumbuli mkoani Tanga ambaye pia ni Waziri wa Zamani wa Ofisi hiyo, Mhe. Januari Makamba (wapili kushoto) walipokutana katika Kikao cha Kwanza cha Mkutano wa 16 wa Bunge leo jijini Dodoma tarehe 3 Septemba 2019. Kulia ni Mbunge wa Kibaha, Mhe. Sylivester Koka.[/caption] [caption id="attachment_46450" align="aligncenter" width="1000"] Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Miraji Mtaturu akiuliza swali la nyongeza wakatiwa kikao cha kwanza cha Mkutano wa 16 wa Bunge leo tarehe 3 Septemba 2019 jijini Dodoma. Mbunge huyo ameapishwa leo baada ya kupita bila kupingwa katika uchaguzi mdogo uliofanyika kutokana na nafasi kuwa wazi baada ya aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo kukosa sifa ya kuendelea na Ubunge.[/caption] [caption id="attachment_46451" align="aligncenter" width="1000"] Baadhi ya wananchi wa Jimbo la Singida Mashariki waliomsindikiza Mbunge wao Mhe. Miraji Mtaturu kushuhudia hafla ya kuapishwa kwake wakipunga mikono baada ya kutambulishwa Bungeni katika Mkutano wa 16 wa Bunge kikao cha kwanza leo tarehe 3 Septemba 2019 jijini Dodoma. Mhe. Mtaturu amesindikizwa na zaidi ya wananchi 200 kutoka jimboni kwake. (Picha na Idara ya Habari – MAELEZO)[/caption]