[caption id="attachment_53363" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akifafanua jambo wakati akifungua mkutano wa pili wa kujadili namna ya kurahisisha usafirishaji wa minofu ya samaki kutokea Kiwanja cha Ndege cha Mwanza uliofanyika jijini Dodoma. Kikao hicho kimewakutanisha viongozi wakuu wa Wizara tano kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,VIwanda na Biashara, Fedha na Mipango, Mambo ya Nje ya Nchi, Mifugo na Uvuvi na Kilimo.[/caption]
Na Mwandishi Wetu- Dodoma
Serikali imewaahidi wafanyabiashara wa minofu ya samaki kuongeza idadi ya mashirika ya ndege yatakayosafirisha mzigo huo ili kuwafikia walaji kwa wakati.
Kauli hiyo imetolewa jijini Dodoma na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, wakati wa kikao cha pili kilichowakutanisha Mawaziri wa Wizara tano zikiwemo Wizara za Mifugo na Uvuvi, Mambo ya Nje ya Nchi, Viwanda na Biashara, Fedha na Mipango na Kilimo.
“Mpaka sasa kuna mashirika zaidi ya mawili ambayo tunafanya mazungumzo nao ili kuleta ndege mkoani Mwanza, hivyo changamoto zilizojitokeza baada ya kuanza usafirishaji huo zinaendelea kushughulikiwa’, amesema Mhandisi Kamwelwe.
[caption id="attachment_53368" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Huduma za Uchukuzi (Uchukuzi), Mhandisi Aron Kisaka (kushoto), akizungumza na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Mhandisi Julius Ndyamukama wakati walipokutana kujadili namna ya kurahisisha usafirishaji wa minofu ya samaki kutokea Kwanja cha Ndege cha Mwanza jijini Dodoma.[/caption]Waziri Mhandisi Kamwelwe, amesema baadhi ya changamoto ambazo zimeshashughulikiwa mpaka sasa ni pamoja na kuanza kwa ujenzi wa uzio na maboresho ya jengo la kutunzia mizigo.
Aidha, Waziri Mhandisi Kamwelwe amesema pamoja na jitihada hizo Wizara kupitia kamati iliyoundwa inaendelea kutafuta masoko ya samaki ili kufikia lengo la kusafirisha tani zaidi ya 100 kwa safari moja.
Kwa upande wake Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhanga Mpina, amesema pamoja na mzigo wa samaki na mabondo tayari uzalishaji wa bidhaa za nyama umeanza na wizara imejipanga kuhakikisha mzigo huo unasafirishwa nje ya nchi ili kuongeza pato la Taifa na wafanyabiashara wa bidhaa hiyo mkoani Mwanza.
“Kwa Mkoa wa Mwanza peke yake uzalishaji wa nyama umeanza na matarajio ni kusafirisha zaidi ya tani hamsini kwa safari moja, kama Wizara tumejipanga vizuri kwenye jambo hili na huo ni mwanzo tu”, mesema Mpina.
[caption id="attachment_53367" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Idara ya Uvuvi, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Emmanuel Bulayi, akifafanua jambo katika kikao cha cha pili cha kujadili namna ya kurahisisha usafirishaji wa minofu ya samaki kutokea Kiwanja cha Ndege cha Mwanza jijini Dodoma.[/caption]Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,John Mongela ameishukuru Serikali kwa kushughulikia changamoto zilizojitokeza na kuahidi kuendelea kuhamasisha viwanda kuzalisha zaidi ili kuongeza pato na kuongeza ajira kwa wanaMwanza.
Katibu Mkuu wa Sekta ya Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho amesema toka kuanza kwa usafirishaji huo mapema Aprili 22, mwaka huu, mpaka sasa tani zaidi ya 140 zimeshasafirishiwa ambapo mpango ni kusafirisha zaidi ya tani 100 kwa safari moja.
[caption id="attachment_53366" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu (LATRA), Bw. Gilliard Ngewe (kulia), akiteta na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Mhandisi Julius Ndyamukama, wakati wa mkutano wa pili wa kujadili namna ya kurahisisha usafirishaji wa minofu ya samaki kutokea Kiwanja cha Ndege cha Mwanza uliofanyika jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_53365" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akizungumza na Naibu Waziri wa Kilimo, Omary Mgumba, wakati wa mkutano wa pili wa kujadili namna ya kurahisisha usafirishaji wa minofu ya samaki kutokea Kiwanja cha Ndege cha Mwanza uliofanyika jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_53364" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu (Sekta ya Uchukuzi), Dkt. Leonard Chamuriho, akifafanua jambo kwa wataalam (hawapo pichani) wakati wa kikao cha pili cha kujadili namna ya kurahisisha usafirishaji wa minofu ya samaki kutokea Kiwanja cha Ndege cha Mwanza jijini Dodoma. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Mifugo na Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah.[/caption]Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.