Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali kujenga Miradi ya Maji 49 Mkoani Pwani
Jan 31, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Daudi Manongi,PWANI

Serikali imepeleka shilingi Bilioni 10.9 ambazo zinatumika kujenga miradi 49 ya maji mkoani Pwani.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa wakati akitoa taarifa ya Serikali kupitia vyombo vya habari Kibaha,Pwani.

“Kati yake miradi 37 ni ya ukarabati, miradi 17 ni mipya. Tayari miradi 7 imeshakamilika na kuanza kutumika na iliyobaki imekamilishwa mwezi huu. Fedha za kutekeleza miradi hii zilianza kutolewa katika Bajeti ya Mwaka 2020/21”, amesema Msigwa.

Amesema kuwa Wananchi wq Pwani takriban laki moja watanufaika na miradi iyo pia katika mwaka huu wa fedha 2021/22, Serikali imeleta Pwani shilingi Bilioni 21.447 ambazo zinatekeleza miradi takribani 54. Miradi hii ikikamilika, tutafikisha maji kwa wananchi kwa asilimia 10.1 zaidi.

juhudi hizo zimeuwezesha Mkoa wa Pwani kuwa na jumla ya miradi 417 ya maji ambayo imewawezesha wana Pwani kupata maji kwa wastani wa asilimia 86.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi