Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Kuendelea Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji Nchini
Dec 24, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_25589" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa Faustin Kamuzora akifurahia maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa SAGCOT Geoffrey Kirenga wakati alipotembelea shamba la mahindi la Kiwanda cha Kuzalisha Viranga na chakula cha Kuku, Silverlands mkoani Iringa, wengine ni Mkurugenzi wa Mashamba na Mifugo Kiwanda cha, Rob Nethersole na Mratibu wa SAGCOT Ofisi ya Waziri Mkuu, Girson Ntimba.[/caption]

Na. Mwandishi Maalum.

Katika moja ya jitihada za kuhakikisha mafanikio ya mkakati wa kujenga Uchumi wa Viwanda nchini serikali imeendelea Kuboresha mazingira bora ya biashara kwa  wawekezaji kwa kuendeleza kilimo ili kuchochea maendeleo na sekta ya kilimo kupitia Mpango wa uendelezaji kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT).

Akizungumza baada  ziara ya Kukagua shughuli za SAGCOT mkoani Iringa kwa kutembelea kiwanda cha kuzalisha vifaranga na chakula cha kuku Silverlands na kiwanda cha kusindika Maziwa cha Asas Diary Milk,   Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa Faustin Kamuzora alifafanua kuwa njia ya kuliwezesha Taifa kuwa na uchumi imara utakaohimili ushindani katika masoko ya kikanda na kimataifa ni kuboresha mazingira ya Uwekezaji.

[caption id="attachment_25590" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa Faustin Kamuzora akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha uendelezaji kilimo Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT), Geoffrey Kirenga wakati alipotembelea shamba la mahindi la Kiwanda cha Kuzalisha Viranga na chakula cha Kuku, Silverlands mkoani Iringa.[/caption] [caption id="attachment_25591" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa Faustin Kamuzora akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Kusindika Maziwa, Asas Diary Milk, Fuad Faraj, wakati alipofanya ziara mkoani Iringa, kukagua viwanda vinavyofanya kazi na Kongani ya Ihemi inayotekelezwa na Mpango wa uendelezaji kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT) unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.[/caption]

“Tunaweka  mazingira wezeshi ya kisera na kisheria ili kuhakikisha ukuaji endelevu wa kiuchumi katika sekta ya kilimo hasa kwa kuishirikisha sekta binafsi na kuhakikisha kilimo kinakuwa na tija, tunao Mpango wa SAGCOT tunataka kutumia fursa hizi katika kilimo kukuza uchumi, tuondokane na kilimo cha kujikimu na kuhamia kilimo biashara. Wawekezaji wanahitaji kuona utayari wa wakulima ili wawekeze. Tukumbuke  zaidi ya asilimia 70 ya malighafi za viwanda zinatokana na kilimo”, alisema Kamuzora.

Naye Katibu Tawala wa mkoa wa Iringa ,Wamoja Ayoub, alifafanua kuwa tayari mkoa huo umeanza kupata mafanikio kwa utekelezaji wa SAGCOT mkoani  humo kwa wakulima kuweza kulimochenye tija , kuongeza thamani mazao yao na kupata masoko ya uhakika.

“Kutokana na ongezeko la matumizi sahihi ya pembejeo kumekuwa na ongezeko la tija kwa mazao kutoka tani 2.2 za mahindi kwa hekta kwa msimu wa mwaka 2014/2015 hadi tani 2.7 za mahindi kwa hekta kwa msimu  wa mwaka 2016/2017na Mpunga kutoka tani 3.2 kwa msimu wa mwaka 2014/2015 hadi tani 4.6 kwa msimu  wa mwaka 2016/2017”, alisema  Wamoja.

[caption id="attachment_25592" align="aligncenter" width="750"] Sehemu ya mitambo ya Kiwanda cha Kuzalisha Viranga na chakula cha Kuku, Silverlands mkoani Iringa, kiwanda hicho kinahitaji tani 7,000 za Soya kwa siku kwa ajili ya uzalishaji lakini hadi sasa wanapata tani 2,000 kwa siku hivyo kupelekea kiasi kingine kuagizwa kutoka nje ya nchi. Mpango wa uendelezaji kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT) unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu tayari umeanza kuboresha mazingira ya uwekezaji ili wananchi wanufaike na fursa hiyo.[/caption] [caption id="attachment_25593" align="aligncenter" width="750"] Sehemu ya mitambo ya Kiwanda cha Kusindika maziwa, Asas Milk Diary mkoani Iringa, kiwanda hicho kina uwezo wa kusindika lita 50,000 za maziwa kwa siku lakini kinapata lita 20,000 kwa siku. Mpango wa uendelezaji kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT) unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu tayari umeanza kuboresha mazingira ya uwekezaji ili wananchi wanufaike na fursa hiyo.[/caption]

Kwa nyakati tofauti wawekezaji katika Kongani ya Ihemi, Mkurugenzi Mtendaji wa Biashara Kiwanda cha kuzalisha Vifaranga na chakula cha kuku  Silverlands, Sean Johnson na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Kusindika Maziwa Asas Diary Milk, Fuad Faraj, walieleza kuwa ili kuboresha mazingira ya uwekezaji na kupunguza gharama za kufanya biashara, wameiomba serikali kufanya mapitio ya kodi hasa katika uzalishaji wa bidhaa za viwanda.

Wawekezaji hao walibainisha kuwa  serikali itafanikiwa zaidi katika kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara ikiwa kutaanzishwa kituo kimoja cha kufanyia kazi “One stop Centre”  kwa mamlaka zote za  udhibiti, usimamizi na uratibu wa shughuli hizo  kwa Kongani ya Ihemi (Iringa na Njombe).

Pia walishauri serikali kuweka ruzuku katika mbegu za viazi na alizeti za viazi mviringo na ili kuwezesha wakulima wadogo kumudu kununua mbegu bora  zitakazo ongeza uzalishaji na kuchangia malighafi za viwanda vilivyo katika kongani ya Ihemi (Iringa naNjombe)

Awali, akieleza utekelezaji wa Mpango wa uendelezaji kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT), Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha uendelezaji kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT), Geoffrey Kirenga alieleza kuwa wanaendelea kuboresha ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi ili kuweza kuboresha mazingira bora ya uwekezaji na biashara katika kongani ya Ihemi

“Tunaamini kilimo ni fursa  kwani ni  wazi wawekezaji wanategemea kwa kiasi kikubwa mavuno na mazao bora ili kuzalisha bidhaa nzuri. Uchumi wa viwanda unategemea kilimo chenye tija na ninyi mnatuhakikishia kuwepo tija hiyo.”

Programu ya SAGCOT inatekelezwa katika  mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Iringa, Rukwa, Mbeya, Ruvuma, Njombe na Katavi  na imegawanywa katika kongani (cluster) sita za Ihemi (Iringa na Njombe), Rufiji, Kilombero, Mbarali, Ludewa na Sumbawanga. Program hiyo imeanza kutekelezwa mwaka 2011 na mwisho wake mwaka ni 2030. WafadhIli wa SAGCOT ni Serikali ya Tanzania, Shirika la misaada la Uingereza (UKAID), Shirika la misaada la Marekani(USAID), Benki ya Dunia (WBG), Ubalozi wa Norway, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na AGR.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi