Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Kuendelea Kuboresha Huduma Mpaka wa Olaika
Nov 04, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) akijibu swali bungeni jijini Dodoma.
 

Na Farida Ramadhani na Peter Haule, WFM, Dodoma

Serikali imeahidi kuendelea kufuatilia mwenendo wa ukuaji wa shughuli za forodha katika mpaka wa Olaika wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha, hatua itakayoiwezesha Serikali kufanya uamuzi wa kufungua Kituo cha Forodha cha kudumu katika mpaka huo.

Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Ngorongoro, Mhe. Emmanuel Lekishon Shangai, aliyetaka kufahamu wakati ambapo Serikali itajenga Kituo cha Forodha katika mpaka wa Kenya na Tanzania wa Olaika ulioko wilayani Ngorongoro.

Mhe. Chande alisema katika Mwaka wa Fedha 2021/22, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilifanya utafiti katika maeneo yote nchini yenye uhitaji wa Ofisi za kudumu za usimamizi wa kodi ukiwemo mpaka wa Olaika wilayani Ngorongoro.

“Serikali ilibaini kuwa gharama za usimamizi wa shughuli za forodha katika mpaka wa Olaika zitakuwa kubwa ikilinganishwa na kiwango cha ushuru wa forodha unaotarajiwa kukusanywa”, alibainisha Mhe. Chande.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi