Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serikali Itaendelea Kuzichukulia Hatua Kazi za Sanaa Zinazo Kiuka Maadili
Apr 10, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_30093" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harisson Mwakyembe ambapo alieleza mikakati ya serikali ya kuendelea kulinda na kuenzi tamaduni na maadili ya Mtanzania hasa katika sekta ya sanaa nchini, wakati wa kipindi cha maswali na majibu katika mkutano wa kumi na moja wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo mjini Dodoma.[/caption]

Na: Octavian Kimario

WHUSM

Serikali imesema itaendelea kuzichukulia hatua kazi za sanaa ikiwa ni pamoja na nyimbo za wasanii zinazokiuka maadili ili kulinda utamaduni na maadili ya Mtanzania.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe bungeni mjini Domdoma wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Arusha Mhe. Catherine Magige (CCM) aliyetaka kujua ni kwanini siku za hivi karibuni kumeshuhudiwa kufungiwa kwa nyimbo na wasanii.

Waziri Mwakyembe ameeleza kuwa  kila Taifa lina Utamaduni wake na nilazima liulinde kwa udi na uvumba na kwamba kinachofanywa na Serikali siyo vita dhidi ya wasanii bali ni kuhakikisha kuwa serikali inalinda maadili ambayo katika kipindi hiki cha maendeleo ya teknolijia ya habari na mawasiliano  kumekuwa na mmomonyoko mkubwa wa maadili hapa nchini, hivyo Serikali ni lazima ichukue hatua.

Amefafanua kuwa, kinachofanyika hivi sasa hapa nchini ikiwemo kufungia nyimbo za wasanii siyo jambo geni kwani nchi mbalimbali zimekuwa zikiwachukulia hatua za kinidhamu wasanii wao wanapokiuka maadili na utamaduni wa nchi hizo. Akitoa mfano kwa nchi ya Marekani, Dkt. Mwakyembe amesema

“Mwanamuziki Rick Ross ambaye ameimba na Diamond, wiki chache zilizopita amepata matatizo kwa kutoa nyimbo ambao maudhui yake yanajenga picha  ya kwamba anaunga mkono ubakaji, kitendo kilichopelekea nyimbo hiyo kufungiwa mara moja nayeye kuomba radhi”

Akisisitiza hatua hizi za Serikali Waziri Mwakyembe amesema Baba wa Taifa aliwahi kusema Taifa lisilo na utamaduni ni Taifa mfu, hivyo Tanzania haiwezi kukubali kuwa Taifa mfu.

Aidha, Dkt. Mwakyembe amewataka wabunge kuiunga mkono Serikali katika kulinda utamaduni wa Mtanzania kwani yanayotokea Tanzania yanatokea duniani kote. “ Mhe. Naibu Spika viongozi wetu hapa wanalalamika lakini ni kwa sababu dunia ni pana na hawajaelewa kinachotekea maeneo mengine, mfano msanii Davido kutoka nchini Nigeria amefungiwa nyimbo zake mbili na Shirika la Utangazaji la Nigeria (Nigerian Broadcasting Cooperation) mwaka huu kwa kukiuka maadali”

Dkt. Mwakyembe amewataja wasanii wengine mbalimbali duniani waliofungiwa nyimbo zao kwa kukiuka maadili bila wabunge wa nchi hizo kulalamikia sheria zao wenyewe kama vile  Wiz Kid, Nine Ice na Koffi Olomide.

“Sisi wabunge, kazi yetu kubwa ni kuhakikisha jamii inaheshimu na kulinda sheria za nchi” amesisitiza Waziri Mwakyembe.

Naye, Naibu Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akijibu swali la msingi la Mbunge wa Morogoro Kusini Mhe. Prosper Joseph Mbena aliyeitaka Serikali kuunda vyombo vya kusimamia maudhui ya matangazo amesema, Serikali inayo vyombo vya kusimamia Maudhui ya vyombo vya Habari na matangazo. Akivitaja vyombo hivyo amesema ni pamoja na TCRA, Basata na Idara ya Habari Maelezo.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi