Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Serengeti Girls Waendelea Kujifua Kuikabili Ufaransa
Oct 14, 2022
Na Jacquiline Mrisho


Na Shamimu Nyaki


Timu ya Taifa ya Wasichana chini ya miaka 17 (Serengeti Girls) imeendelea na mazoezi Oktoba 13, 2022 Uwanja wa Utorda Goa India.


Serengeti Girls ilianza na mazoezi ya asubuhi katika fukwe zilizopo eneo la Utorda na baadae katika uwanja wa eneo hilo.


Mazoezi hayo ni katika maandalizi ya Mechi dhidi ya Ufaransa itakayochezwa Oktoba 15, 2022 majira ya Saa 4:30 jioni saa za nchini India katika Uwanja wa Pandit Jawaharlal Nehru jijini Goa India.


Katika mazoezi hayo, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Michezo, Bw. Ally Mayay ameendelea kuwapa hamasa wachezaji hao kuwa uwezo wanao wakupambana na kuwakilisha vyema Taifa.

Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu Umri chini ya Miaka 17 (Serengeti Girls) inaendelea na mazoezi ya Mashindano ya Kombe la Dunia yanayoendelea nchini India.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi