Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

RC Tabora Kuwasaka Wanaochoma Moto Misitu na Miti Iliyopandwa
Jun 29, 2018
Na Msemaji Mkuu

Na Tiganya Vincent - Rs Tabora

Watendaji wa ngazi mbalimbali mkoani Tabora wameagiza kuanza zoezi la kuwasaka na kuwakamata watu ambao wamekuwa na tabia ya kuchoma moto ovyo wakati wa maandalizi ya mashamba na wengine kwa ajili ya kutaka nyasi ziote upya kwa ajili ya mifugo.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alitoa kauli hiyo jana wilayani Uyui wakati wa ziara yake katika Kijiji cha Kakola na Msimba akiwa katika kampeni ya kuhimiza wananchi kujiunga na ushirika, kupinga vita utoro na mimba za utotoni.

Alisema, hivi sasa kumeibuka tabia ya watu kuanza kuchoma ovyo moto ambao umekuwa ukisababisha hasara kubwa katika misitu na hata kuunguza miti iliyopandwa hivi karibuni.

Mwanri alisema ni marufuku kuandaa mashamba yao kwa kuchoma moto kwani wamekuwa wakiuacha na kusambaa maeneo mengine na hivyo kuleta athari katika misitu ya asili na viumbe wengine.

Aliwataka wananchi na wakulima mkoani humo kuandaa mashamba kwa njia ya kisasa bila kuathiri mazingira pamoja na viumbe hai wengine hatua ambayo itawezesha kutunza na kuhifadhi mazingira kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo.

Katika kukabiliana na tabia hiyo, Mkuu wa Mkoa huyo amewaagiza watendaji wa vijiji na kata kuhakikisha kwamba wanawachukulia hatua kali za kisheria watu watakaobainika kufanya uharibifu huo kwa kuwa haiwezekani mtu akachoma moto asijulikane .

Alisema katika kijiji au Kata ambayo atakuta watu wamechoma moto na umeteketeza miti iwe ya kupanda au ya asili kiongozi huyo atawajibika kwa kushindwa kusimamia sheria.

Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Mkoa misitu mingi ya asili na miti mingi iliyopandwa katika kipindi cha mvua za masika ipo hatarini kutokana na baadhi ya watu ambao wameanza kuchoma ovyo misitu.

Alitaja sababu  kubwa ya uchomaji moto huu wengine ni kwa sababu ya uvivu wa kuandaa mashamba yao  kwa kupalilia na wengine kuadai kuwa wanapochoma moto wanapata malisho mapya ya mifugo jambo ambao sio rafiki kwa mazingira.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi