Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

RAS Mwanza Awataka Wadau wa Maafa Kuwa na Mikakati ya Kukabiliana na Athari za El Nino
Sep 25, 2023
RAS Mwanza Awataka Wadau wa Maafa Kuwa na Mikakati ya Kukabiliana na Athari za El Nino
Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji, Emily Kasagara akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha kujadili masuala ya maafa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Menejimenti ya Maafa kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa leo tarehe 25 Septemba, 2023 jijini Mwanza..
Na Mwandishi Wetu.

Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji, Emily Kasagara amewataka wadau wa Maafa mkoani Mwanza kujiandaa kwa kina kukabiliana na maafa ya mvua za El Nino zinazotarajiwa kunyesha siku za usoni ili kuwa na namna bora ya kuwalinda na jamii isiangamie.

Ameyasema hayo leo tarehe 25 Septemba, 2023 wakati akifungua kikao kazi cha kujadili masuala ya maafa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Menejimenti ya Maafa kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa, Kasagara amesema, ni lazima kamati za Maafa katika ngazi zote kuwa na mkakati kabambe wa kukabiliana nazo.

Aidha, ametoa wito kwa wadau hao watakaoketi kwa siku mbili za mjadala wa namna ya kukabiliana na majanga kuchangia uzoefu wao na utaalam wao kwa namna gani wanaona inafaa kukabiliana na hali hiyo itakapotokea na wafikishe elimu kwenye jamii ili kujikinga kwa pamoja.

Naye, Mkurugenzi wa Maafa kutoka Idara ya Menejimenti ya Maafa-Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Prudence Costantine, amesema Serikali kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa tarehe 24 Agosti, 2023 ilitoa utabiri ulioonesha kwamba kutakuwa na mvua za wastani na juu ya wastani (El Nino) kwa mikoa kadhaa nchini ukiwemo Mkoa wa Mwanza hivyo ni lazima wadau wajiandae kukabiliana nazo.

"Tunaweza tukapata maafa kama magonjwa na vinginevyo kutokana na mvua hizo na ndio maana ofisi ya Waziri Mkuu ikaona ije na mpango wa kukabiliana na maafa hayo na hadi sasa wataalamu mbalimbali wamesambaa kwenye mikoa mbalimbali kuketi pamoja na kamati za maafa za mikoa hiyo kuona namna ya kukabiliana” ameongeza Costantine.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi