[caption id="attachment_32967" align="alignnone" width="859"] Washiriki wakifuatilia mafunzo kutoka kwa mmoja wa wawezeshaji wa mafunzo hayo (hayupo pichani).[/caption]
Na Nashon Kennedy, Bukoba
SERIKALI mkoani Kagera imeiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kufanya uhakiki wa ukusanyaji wa mapato na matumizi ya mifumo ya kielektroniki ya ukusanyaji wa maoato kwa halmashauri ya wilaya ya Karagwe, baada ya halmashauri hiyo kubainika kushindwa kutumia kikamilifu mifumo hiyo ambayo imewekwa kwa gharama kubwa ya fedha za walipa kodi.
Kauli hiyo imetolewa jana mjini Bukoba na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Diwani Athuman muda mfupi baada ya kufungua mafunzo ya siku nne ya mfumo wa usimamizi wa fedha za umma wa epicor toleo la 10.2 ulioboreshwa ili kuwawezesha kubadilishana taarifa na Mfumo wa Mipango na bajeti, Mfumo wa uhasibu na utoaji wa taarifa za fedha moja kwa moja kwenye vituo vya kutolea huduma (FFARS) kwa waweka hazina na maafisa wasimamizi wa fedha mikoa ya Mara na Kigoma.
“Tumetuma timu maalum ya Mkoa ya Takukuru kwenda wilayani Karagwe kufanya uhakiki wa ukusanyaji wa mapato, kama sehemu ya kuona matumizi ya mifumo hii inatumika vyema”, alisema.
[caption id="attachment_32968" align="alignnone" width="900"]Kufuatia hatua hiyo, Athuman amewaagiza Wakurugenzi watendaji wa halmashauri zote kutekeleza wajibu wao kikamilifu kwa kusimamia na kuitumia vizuri mifumo yote ya serikali iliyofungwa kwenye halmashauri zao ili kuleta ufanisi wa utendaji kazi, utoaji wa taarifa za serikali kwa wakati na ukusanyaji wa mapato ya serikali.
“Iko mifumo mingi ya fedha katika halmashauri zetu ambayo imefungwa kwa gharama kubwa, lakini haitumiwi kwa kiwango kinachotakiwa cha kutuletea tija kwa kutoa huduma na shughuli mbalimbali”, alisema na kuongeza kuwa serikali itahakikisha kunakuwepo na matumizi sahihi ya mifumo ili kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato na utendaji kazi.
Alisema baadhi ya halmashauri nchini zimekuwa dhaifu katika kuitumia mifumo hiyo licha ya serikali na wafadhili kuingia gharama kubwa katika kuifunga, jambo ambalo alisema serikali italivalia njuga ili mifumo hiyo iweze kutumiwa vizuri.
“Kile kinachokusanywa na halmashauri zetu hakitumiki ipasavyo, unakuta halmshauri ina mashine za mfumo lakini zinaweka stoo na watu wanakusanya fedha na kuziweka mfukoni”, alifafanua.
[caption id="attachment_32969" align="aligncenter" width="815"]Akizungumza kwa niaba ya washiriki wenzake, Mweka Hazina wa Halmashauri ya Kakonko mkoani Kigoma Mercy Swai alisema mafunzo hayo yamekuja kwa wakati muafaka na yatawaondolea changamoto za utendaji kazi wa kimfumo zilizokuwepo awali, ambapo kupitia mfumo wa Epicor 10.2 ambao unafanya kazi kwa kuunganishwa na mifumo mingine utawawezesha kufanya kazi kwa ufanisi kwa kutoa taarifa nzuri zinazofanana kwa mifumo yote.
Mfumo wa Epicor 10.2 ambao umeboreshwa yanayofanyika kwa mikoa ya Dodoma, Mwanza, Mtwara na Iringa na mfumo wa mipango na bajeti na ule wa uhasibu na utoaji wa taarifa za fedha za vituo vya kutolea huduma (FFARS) yana lengo la kuwapa uelewa wa mabadiliko na maboresho yaliyofanyika kwenye mfumo watumishi hao wa halmashauri nchini ili kufanya kazi zao kwa ufanisi.