Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Dkt. Rahma Salim Mahfoudh kuwa Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar, hafla hiyo ilifanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.31-01-2022.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Dkt. Mwinyi Talib Haji na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, wamehudhuria katika hafla kuapishwa Viongozi walioteuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kushika nafasi mbali mbali katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.31-01-2022.
Viongozi Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Zanzibar waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Viongozi walioteuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kushika nafasi mbali mbali katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.31-01-2022