Rais wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema Awasili Nchini
Aug 02, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Zambia, Mhe. Hakainde Hichilema mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Terminal one Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Zambia, Mhe. Hakainde Hichilema wakati Nyimbo za Taifa (Tanzania na Zambia) zikipigwa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Terminal one Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Zambia, Mhe. Hakainde Hichilema akikagua Gwaride la Heshima lililoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Terminal one Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Zambia, Mhe. Hakainde Hichilema wakati wakisalimiana na viongozi mbalimbali waliofika kwenye mapokezi katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Terminal one Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Agosti, 2022.