Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Samia Azindua Mkongo wa Mawasiliano wa Baharini na Teknolojia ya Mawasiliano ya Kasi ya 5G ya Airtel
Aug 10, 2023
Rais Samia Azindua Mkongo wa Mawasiliano wa Baharini na Teknolojia ya Mawasiliano ya Kasi ya 5G ya Airtel
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza kwa njia ya Mtandao na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Mkongo wa Baharini cha Airtel 2Afrika pamoja na Mtandao wenye kasi ya 5G wa Kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania iliyofanyika Mbezi Tanki Bovu Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Agosti, 2023.
Na Ikulu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kuashiria uzinduzi wa Kituo cha Mkongo wa Baharini cha Airtel 2Afrika kilichopo Mbezi Tanki Bovu jijini Dar es Salaam tarehe 10 Agosti, 2023. Wengine pichani ni Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila, Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Airtel Afrika, Dkt. Olusegun Ogunsanya, Mtendaji Mkuu wa Airtel Tanzania, Dinesh Balsingh pamoja na viongozi wengine wakishuhudia.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amevaa Kifaa Maalum cha kumuwezesha kuona kwa ukaribu matukio mbalimbali duniani kijulikanacho kama Teknolojia Ukweli Halisi (Virtual Reality Device) mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Mkongo wa Mawasiliano Baharini cha Kampuni ya Airtel Tanzania kilichopo Mbezi Tanki Bovu Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Agosti, 2023. Wengine katika picha ni Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye pamoja na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano na Simu za Mkononi ya Airtel Tanzania, Dinesh Balsingh wakishuhudia tukio hilo.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa pamoja na viongozi wengine wakati akimsikiliza Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye kuhusu Mkongo wa Mawasiliano wa Baharini wa Airtel2Afrika kabla ya kuuzindua katika Kituo hicho cha Kampuni ya Mawasiliano na Simu za Mkononi ya Airtel Tanzania kilichopo Mbezi Tanki Bovu jijini Dar es Salaam tarehe 10 Agosti, 2023.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akibonyeza Kitufe kuashiria uzinduzi wa Mtandao wenye kasi ya 5G wa Kampuni ya Airtel Tanzania katika hafla iliyofanyika katika Kituo cha Mkongo wa Mawasiliano Baharini cha Kampuni ya Airtel Tanzania kilichopo Mbezi Tanki Bovu Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Agosti, 2023.

 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea mfano wa nembo ya 5G kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Airtel Afrika, Dkt. Olusegun Ogunsanya mara baada ya uzinduzi uliofanyika Mbezi Tanki Bovu jijini Dar es Salaam tarehe 10 Agosti, 2023.

 

 

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi