Rais Samia Aweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Kituo cha pamoja cha Forodha Kasumulu, Azindua Barabara ya Kikusya-Ipinda-Matema km 39
Aug 07, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Wananchi wa Kasumulu baada ya kuweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Kituo cha pamoja cha Forodha Kasumulu wilayani Kyela mkoani Mbeya tarehe 07 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa pamoja na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Kikusya-Ipinda-Matema km 39 katika hafla fupi iliyofanyika Ipinda, Kyela Mkoani Mbeya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Ipinda, Kyela baada ya kufungua Barabara ya Kikusya-Ipinda-Matema km 39 katika hafla fupi iliyofanyika Ipinda, Kyela mkoani Mbeya tarehe 07 Agosti, 2022.