Rais Samia Awatunuku Kamisheni Maafisa Wanafunzi 740
Nov 26, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Sehemu ya Maafisa Wanafunzi 740 wakivalishana vyeo mara baada ya kutunukiwa Kamisheni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan katika viwanja vya Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi - Monduli mkoani Arusha leo tarehe 26 Novemba, 2022.
Sehemu ya Maafisa Wanafunzi 740 wakila Kiapo cha Utii kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan katika viwanja vya Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi - Monduli mkoani Arusha leo tarehe 26 Novemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri kwenye mafunzo wakati wa hafla ya kutunuku Kamisheni Maafisa Wanafunzi 740 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi - Monduli mkoani Arusha leo tarehe 26 Novemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshima la Maafisa Wanafunzi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kabla ya kuwatunuku Kamisheni kuwa Maofisa katika Cheo cha Luteni Usu katika hafla iliyofanyika viwanja vya Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi - Monduli mkoani Arusha leo tarehe 26 Novemba, 2022.
Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi, Brigedia Jenerali Jackson Mwaseba akizungumza wakati wa hafla ya kutunuku Kamisheni Maafisa Wanafunzi 740 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi - Monduli mkoani Arusha leo tarehe 26 Novemba, 2022
Wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya utoaji wa Kamisheni kwa Maafisa wanafunzi wa Jeshi la Wanafunzi wa Tanzania katika viwanja vya Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi - Monduli mkoani Arusha leo tarehe 26 Novemba, 2022.