Rais Samia Awaongoza Watanzania Sensa ya Watu na Makazi
Aug 23, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango pamoja na mke wake Mbonimpaye Mpango wakizungumza na Karani wa Sensa, Isack Mgosho wakati walipokuwa wakihesabiwa kwenye Sensa ya Watu na Makazi katika Makazi yao Chanika Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi, wakimsikiliza Karani wa Sensa ya Watu na Makazi, Bi. Asia Hassan Mussa wakati wa zoezi la kuhesabiwa lililofanyika katika makaazi yake Migombani Ikulu ndogo leo 23-8-2022, zoezi hilo la Sensa ya Watu na Makazi limeanza leo kwa pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihojiwa na kutoa majibu ya dodoso kuu la Sensa ya Watu na Makazi kwa Karani wa Sensa, Amina Mwambe wakati alipokuwa akihesabiwa katika makazi yake yaliyopo katika Kijiji cha Nandagala, Ruangwa mkoani Lindi Agosti 23, 2022.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa akizungumza na Karani wa Sensa ya Watu na Makazi, Spencia Rutalemwa wakati akihesabiwa nyumbani kwake kijiji cha Ahakishaka, Kata ya Nyabiyonza, wilaya ya Karagwe, mkoani Kagera.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza na Karani wa Sensa, Jumanne Marko katika Sensa ya Watu na Makazi nyumbani kwake Kimani, Kisarawe, Pwani leo 23-08-2022, aliwasihi wananchi kushiriki kwa kutoa taarifa sahihi.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akizungumza na Karani wa Sensa ya Watu na Makazi, Bwana Samora Benet Lugenge wakati alipokuwa akihesabiwa katika Makazi yake Mtama Lindi leo kwenye Sensa ya Watu na Makazi.
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akizungumza na Karani wa Sensa ya Watu na Makazi wakati alipokuwa akihesabiwa katika Makazi yake jijini Dodoma
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima akiwa na mume wake Adv. Gwajima, wamehesabiwa katika makazi yao Sala Sala jijini Dar es Salaam wakati wa zoezi la Sensa ya Watu na Makazi zoezi lililoanza leo Agosti 23, 2022
Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko akijibu maswali aliyoulizwa na Karani wa Sensa ya Watu na Makazi, Magera Kilosa wakati akihesabiwa nyumbani kwake Kata ya Bulangwa Wilaya ya Bukombe, mkoani Geita leo tarehe 23 Agosti, 2022