Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika Mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliomalizika leo Agosti 18 katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Bingu uliopo Jijini Lilongwe nchini Malawi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangangwa pamoja Mwenyekiti wa SADC Rais wa Malawi Mhe. Lazarus McCathy Chakwera wakati wakitoka kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Bingu uliopo Jijini Lilongwe nchini Malawi mara baada ya Mkutano huo leo Agosti 18, 2021.