Kamishna Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU), Salum Hamduni akimkabidhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mlezi wa Chama cha Skauti Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan Mwongozo wa kuwawezesha na kuwafundisha vijana wa Skauti jinsi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Nchini, kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mlezi wa Skauti Tanzania yaliyoadhimishwa Oktoba 02, 2021 katika Viwanja vya Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mlezi wa Chama cha Skauti Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia katika Maadhimisho ya Siku ya Mlezi wa Skauti Tanzania yaliyoadhimishwa leo Oktoba 02, 2021 katika viwanja vya Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mlezi wa Chama cha Skauti Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimvisha tuzo Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Simai Mohammed Said kwa kutambua mchango wake katika kuunga mkono Skauti Tanzania kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mlezi wa Skauti Tanzania yaliyofanyika Oktoba 02, 2021 katika viwanja vya Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mlezi wa Chama cha Skauti Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimvisha tuzo Kamishna Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU), Salum Hamduni kwa kutambua mchango wake katika kuunga mkono Skauti Tanzania katika Maadhimisho ya Siku ya Mlezi wa Skauti Tanzania yaliyoadhimishwa Oktoba 02, 2021 katika Viwanja vya Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.