Rais Samia Ashiriki Kikao Kazi cha Wakuu wa Mikoa kuhusu Mfumo wa Anwani za Makazi nchini
Feb 08, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Convention Centre Jijini Dodoma kwa ajili ya kuhudhuria Kikao Kazi cha Wakuu wa Mikoa kuhusu Mfumo wa Anwani za Makazi nchini leo tarehe 08 Februari, 2022. Wengine katika picha ni Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa pamoja na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla
Wakuu wa Mikoa, Mawaziri pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwa katika Kikao Kazi cha Wakuu hao wa Mikoa kuhusu Mfumo wa Anwani za Makazi kilichofanyika katika ukumbi wa Mkutano wa Jakaya Kikwete Convention Centre Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 08 Februari, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wakuu wa Mikoa, Mawaziri pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali wakati wa Kikao Kazi cha Wakuu wa Mikoa kuhusu Mfumo wa Anwani za Makazi kilichofanyika katika ukumbi wa Mkutano wa Jakaya Kikwete Convention Centre Jijini Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akishuhudia Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akipokea kwa niaba yake Bango lenye Anwani ya Makazi ya Ofisi ya Rais, Ikulu mara baada ya kuzungumza katika Kikao Kazi cha Wakuu wa Mikoa kuhusu Mfumo wa Anwani za Makazi kilichofanyika katika ukumbi wa Mkutano wa Jakaya Kikwete Convention Centre Jijini Dodoma