Rais Samia Amuapisha Mhe. Angeline Mabula kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Feb 09, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan akishuhudia Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angeline Mabula akila Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 09 Februari, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akisikiliza jambo kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Tulia Ackson mara baada ya hafla ya Uapisho iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angeline Mabula mara baada ya kumuapisha katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 09 Februari, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Ikulu, Dkt. Moses Kusiluka, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson katika picha ya pamoja na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angeline Mabula mara baada ya kumuapisha katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 09 Februari, 2022.