Rais Samia Amuapisha Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza na Majaji wa Mahakama Kuu
Aug 29, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia Viongozi mbalimbali mara baada ya kumuapisha Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) Mzee Ramadhani Nyamka pamoja na Majaji Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 29 Agosti, 2022.
Majaji wa Mahakama Kuu pamoja na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP), Mzee Ramadhani Nyamka wakiweka Saini kwenye viapo vyao vya Maadili Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 29 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Phillip Isdor Mpango, Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro, Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Hamis Juma, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Kattanga pamoja na Majaji wa Mahakama Kuu aliowaapisha Ikulu mkoani Dodoma tarehe 29 Agosti, 2022.