Rais Samia Amuapisha Balozi wa Tanzania Nchini Kuweit na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi
Jan 13, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Ndugu. Said Shaibu Mussa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kuwait katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino, Mkoani Dodoma leo tarehe 13 Januari 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Ndugu. Aisha S. Amour Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) kushoto na Ndugu. Said Shaibu Mussa Balozi wa Tanzania nchini Kuwait kulia, mara baada ya kuwaapisha katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino, Mkoani Dodoma leo tarehe 13 Januari 2022.