Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Samia Akutana na Kuzungumza na Viongozi wa Kampuni ya Kimataifa ya Power Holding, Doha nchini Qatar
Oct 03, 2023
Rais Samia Akutana na Kuzungumza na Viongozi wa Kampuni ya Kimataifa ya Power Holding, Doha nchini Qatar
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika Kikao na ujumbe wa Kampuni ya Kimataifa ya Power Holding kuhusu maeneo mbalimbali ya Uwekezaji nchini Tanzania. Kikao hicho kilifanyika katika Ofisi za Kampuni hiyo inayojihusisha na masuala kadhaa ikiwemo Ujenzi, Kilimo na Utalii, Doha nchini Qatar tarehe 03 Oktoba, 2023.
Na Ikulu

Viongozi mbalimbali wakifuatilia mawasilisho yaliyokuwa yakitolewa na viongozi wa Kampuni ya Kimataifa ya Power Holding kuhusu Uwekezaji wanaoufanya katika maeneo mbalimbali Duniani, Doha nchini Qatar tarehe 03 Oktoba, 2023. 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika Kikao na ujumbe wa Kampuni ya Kimataifa ya Power Holding inayojihusisha na masuala kadhaa ikiwemo Ujenzi, Kilimo na Utalii kuhusu maeneo mbalimbali ya Uwekezaji nchini Tanzania. Kikao hicho kilifanyika katika Ofisi za Kampuni hiyo zilizopo Doha nchini Qatar tarehe 03 Oktoba, 2023.

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Gilead Teri akizungumza kuhusu fursa mbalimbali za Uwekezaji zilizopo nchini Tanzania kwenye kikao pamoja na viongozi wa Kampuni ya Kimataifa ya Power Holding kilichofanyika Doha nchini Qatar tarehe 03 Oktoba, 2023. 

 

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi