Rais Samia Akutana na Kuzungumza na Makamu wa Rais Mtendaji wa Kampuni ya Equinor
Aug 24, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Makamu wa Rais Mtendaji wa Kampuni ya Equinor inayoshughulikia utafiti na uzalishaji wa Mafuta na Gesi Kimataifa, Bw. Al Cook mara baada ya kuwasili Ikulu Chamwino jijini Dodoma tarehe 24 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais Mtendaji wa Kampuni ya Equinor inayoshughulikia utafiti na uzalishaji wa Mafuta na Gesi Kimataifa, Bw. Al Cook (wa sita kutoka Kushoto) ambaye aliambatana na ujumbe wake pamoja na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Shell (Tanzania) Bw. Jared Kuehl wa pili kutoka kulia katika picha ya pamoja mara baada ya mazungumzo yao Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 24 Agosti, 2022