Rais Samia Akutana na kuzungumza na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Mhe. Patricia Scotland, Ikulu Tunguu Zanzibar
May 05, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth), Mhe. Patricia Scotland mara baada ya kuwasili Ikulu Tunguu, Zanzibar tarehe 05 Mei, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Azimio la Jumuiya ya Madola (Charter of the Commonwealth) kutoka kwa Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Mhe. Patricia Scotland mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu Tunguu, Zanzibar tarehe 05 Mei, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Mhe. Patricia Scotland mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu Tunguu, Zanzibar tarehe 05 Mei, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Mhe. Patricia Scotland aliyeambatana na Ujumbe wake Ikulu Tunguu, Zanzibar tarehe 05 Mei, 2022.