Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Samia Ahutubia Ufunguzi Jengo la Kitega Uchumi (Safina House)
Aug 15, 2023
Rais Samia Ahutubia Ufunguzi Jengo la Kitega Uchumi (Safina House)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali pamoja na Waumini wa Kanisa la Anglikana Tanzania mara baada ya kufungua Jengo la Kitega Uchumi (Safina House) la Kanisa hilo katika sherehe zilizofanyika kwenye viwanja vya Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu Jijini Dodoma tarehe 15 Agosti, 2023.
Na Ikulu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT), Dkt. Dickson Chilongani wakati wakiwa kwenye eneo lenye michoro ya jengo la Kitega Uchumi (Safina House) la Kanisa hilo Jijini Dodoma tarehe 15 Agosti, 2023.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya Kitabu (Itifaki ya Biblia) kutoka kwa Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT) Dkt. Dickson Chilongani mara baada ya kufungua Jengo la Kitega Uchumi (Safina House) la Kanisa hilo Jijini Dodoma tarehe 15 Agosti, 2023.

 

 

 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Maaskofu wa Kanisa la Anglikana Tanzania wakati akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Jengo la Kitega Uchumi (Safina House) la Kanisa hilo kwenye sherehe zilizofanyika katika viwanja vya Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu Jijini Dodoma tarehe 15 Agosti, 2023.
Muonekano wa Jengo la Kitega Uchumi (Safina House) la Kanisa la Anglikana Tanzania, Dayosisi ya Central Tanganyika ambalo limefunguliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja vya Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu tarehe 15 Agosti, 2023.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi