Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisaini kitabu cha kumbukumbu katika ofisi za Umoja wa Mataifa Jijini New York Marekani mara baada ya kuhutubia mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo Septemba 23, 2021. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Antonio Guterres katika Ofisi za Umoja wa Mataifa Jijini New York Nchini Marekani leo Septemba 23, 2021.