Rais Samia Ahutubia Kwenye Maadhimisho ya miaka 10 ya NDC
Sep 08, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan akikabidhiwa Cheti kama ishara ya kutunukiwa Tuzo ya Heshima ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania (NDC) na Mkuu wa Chuo hicho, Meja Jenerali Ibrahim Michael Mhona kwenye maadhimisho ya miaka 10 ya Chuo hicho Kunduchi Jijini Dar es Salaam tarehe 08 Septemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan akipewa Tuzo ya Heshima ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania (NDC) na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Tax kwenye maadhimisho ya miaka 10 ya Chuo hicho yaliyofanyika Kunduchi Jijini Dar es Salaam tarehe 08 Septemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na washiriki waliohudhuria kwenye maadhimisho ya miaka 10 ya Chuo hicho yaliyofanyika Kunduchi Jijini Dar es Salaam tarehe 08 Septemba, 2022.