Rais Samia Afunga Maonesho ya Nane Nane mwaka 2022
Aug 08, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akilihutubia Taifa kwenye kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane Kitaifa ambayo imefanyika katika Viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya tarehe 08 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua na kuangalia vifaa mbalimbali vya shughuli za ufugaji wa ng’ombe vilivyopo katika banda la Asas kwenye kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane Kitaifa ambayo imefanyika katika Viwanja vya John Mwakangale - Mbeya.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mfumo wa ruzuku ya Mbolea mara baada ya kutembelea Mabanda na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na wadau wa Kilimo kwenye kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akikabidhi mfano wa funguo za Trekta kwa ajili ya wakulima bora ambao wamepewa zawadi kutokana na mafanikio waliyopata katika kilimo kwenye kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane