Rais Samia Afanya Ziara ya Kikazi Bunda na Butiama Mkoani Mara
Feb 07, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Makongoro Nyerere ambaye ni mtoto wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakati akielekea katika kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kuweka shada la maua Butiama mkoani Mara leo tarehe 07 Februari, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Makongoro Nyerere ambaye ni mtoto wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Ally Hapi mara baada ya kuweka shada la maua katika kaburi hilo la Baba wa Taifa Butiama mkoani Mara leo tarehe 07 Februari, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Butiama mkoani Mara wakati akielekea Bunda mkoani humo leo tarehe 07 Februari, 2022.
Sehemu ya Wananchi wa Butiama wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati akizungumza nao leo tarehe 07 Februari, 2022.