Rais Samia Aelekea Nchini Ufaransa kwa Ziara ya Kikazi
Feb 09, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango pamoja na Rais wa Zanzibar, Mhe. Husein Ali Mwinyi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Karume Zanzibar kabla ya kuondoka kuelekea nchini Ufaransa leo tarehe 09 Februari, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Wazee wa Zanzibar waliofika katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Karume kabla ya kuondoka na kuelekea nchini Ufaransa leo 09 Februari, 2022.