Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Museveni Aishukuru Tanzania Kuwezesha Mradi wa Bomba la Mafuta
Nov 12, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_22377" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni , Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga wakiangalia Jiwe la Msingi. Wengine ni Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini Mhandisi Irene Muloni na Viongozi mbalimbali.[/caption]

Na: Asteria Muhozya, Hoima

 Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kukubali kutumia barabara zake kwa ajili ya Ujenzi wa Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga, Tanzania, pamoja na kuweka mazingira wezeshi ya utekelezaji wa mradi husika.

Rais Museveni aliyasema hayo tarehe 11 Novemba, 2017, wakati wa Sherehe za Uwekaji Jiwe la Msingi kwa Upande wa Uganda zilizofanyika Hoima nchini Uganda. Awali sherehe kama hizo kwa upande wa Tanzania zilifanyika eneo la Chongoleani Jijini Tanga tarehe 5 Agosti,2017, mahali ambapo kutajengwa gati ya kushusha mafuta.

[caption id="attachment_22378" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni akizungumza jambo wakati wa Sherehe za Uwekaji Jiwe la Msingi Kwa Upande wa Uganda Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi Kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga Tanzania.[/caption] [caption id="attachment_22379" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni katika picha ya Pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga ambaye amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli katika sherehe hizo, (wa tatu kutoka kulia) Balozi wa Tanzania nchini Uganda Grace Mgovano ( wa kwanza kulia) Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (wa pili kulia) na Wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).[/caption]

Eneo la Hoima ndipo kitajengwa Kiwanda cha Kusafisha Mafuta kabla ya kusafirishwa kwenda nchini Tanzania. Pia Hoima ndiyo eneo ambalo mafuta yataanza kusafirishwa kuelekea Bandari ya Tanga Tanzania kabla ya kusafirishwa katika  soko la kimataifa.

Rais Museveni alieleza kuwa, kugundulika kwa Mafuta nchini Uganda kumechangiwa na mafunzo  ya yaliyotolewa kwa  Wataalam wazawa wa nchi hiyo ambao wamechangia kugundulika kwa mafuta nchini humo.

Aidha, Rais Museveni alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wazazi na wanafunzi kujikita katika masomo ya sayansi ili waweze kusimamia  na kuendeleza shughuli za mafuta nchini humo kwa maendeleo ya nchi hiyo.

[caption id="attachment_22380" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Viwanda wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akizungumza jambo, Wanaofuatialia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga (wa pili kulia), Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda Mhandisi Irene Muloni na mshehereshaji.[/caption] [caption id="attachment_22381" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (kulia), Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Mafuta wa Uganda Irene Muloni (katikati) na Mshehereshaji wa Sherehe za Uwekaji Jiwe la Msingi Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga kwa upande wa Uganda wakisalimia hadhara iliyohudhuria sherehe hizo.[/caption]

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, alisifu Jitihada za Rais Museveni katika kuendeleza utafiti  bila kukata tamaa na hatimaye kufanikisha ugunduzi wa mafuta nchini humo kwa kuwatumia Wataalam wa ndani.

Balozi Mahiga alimwelezea Rais Museveni kuwa ni Rais ambaye ametoa mfano wa kutokubali kushindwa kutokana na namna historia ya utafiti wa mafuta nchini humo ilivyokuwa na kuongeza kuwa, amekuwa mfano  na alama ya namna ya kuwatumia wataalam wa ndani katika kuendeleza rasilimali za nchi kutokana na ugunduzi huo.

Aliongeza kuwa, manufaa ya ujenzi wa bomba hilo si tu kwa Uganda  bali pia  kwa Afrika Mashariki na kwamba ugunduzi huo umewezesha kupatikana kwa  rasimali ya thamani iliyofichika katika Bonde la Ufa  ambayo inakuwa ya manufaa kwa  nchi hizo na Afrika.

[caption id="attachment_22382" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga ambaye amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli katika Sherehe za Uwekaji Jiwe la Msingi Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi kwa Upande wa Uganda akisalimiana na Viongozi mbalimbali wakati akiingia eneo la Sherehe.[/caption] [caption id="attachment_22383" align="aligncenter" width="750"] Naibu Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Maleko Nderimo, akizungumza jambo na Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini Mhandisi Irene Muloni wakati wa Sherehe za Uwekaji Jiwe la Msingi Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi zilizofanyika Hoima nchini Uganda.[/caption]

"Nimemjua Museveni tangu akiwa kijana mdogo mwerevu, shupavu na mtu mwenye matarajio makubwa na kiongozi thabiti. Katika hili la ugunduzi nashawishika kusema Uganda wana kila sababu ya kujivunia kiongozi huyu. Ni katika kipindi kirefu nchi inaweza kupata kiongozi bora," aliongeza Dkt. Mahiga.

Awali, akizungumza  katika sherehe hizo, Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini  wa Uganda Irene Muloni  alisema kuwa, ugunduzi huo umewezesha nchi ya Uganda kupata Mwaliko kutoka Jumuiya ya Nchi zinazozalisha Mafuta  Duniani (OPEC) wa kuhudhuria mkutano wa nchi  hizo kutokana na ugunduzi wa mafuta nchini humo.

Muloni aliongeza kuwa, utekelezaji wa mradi huo unatokana na msukumo na dhamira ya dhati ya Marais wa Uganda na Tanzania kwa kuhakikisha kwamba mradi husika unatekelezwa na kuongeza kuwa, mradi huo utawezesha kupatikana kwa ajira takribani  10,000 wakati wa ujenzi na utawezesha ajira mpya zipatazo 1,600.

[caption id="attachment_22384" align="aligncenter" width="750"] Mfalme wa Bunyoro , Ufalme wa Kitara, Rukirabasanja Solomon Nguru, akisalimiana na mmoja wa Mawaziri wa nchini Uganda. Kushoto Malkia.[/caption] [caption id="attachment_22385" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga akihutubia wananchi wa hadhira kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli.[/caption]

Nae Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani aliueleza  mradi huo kuwa, utahusisha ujenzi wa Bomba la urefu wa kilomita 1145, ujenzi wa vituo 6, vinne vikiwa vya kusukuma mafuta na viwili vya kupunguza kasi ya mafuta na ujenzi wa matanki 5 yenye uwezo wa kubeba mapipa  500,000  kila moja na ujenzi wa vali (valve) 53  za kufunga bomba.

Historia ya shughuli za utafiti Uganda inaonesha kuwa, shughuli za utafiti wa mafuta nchini humo zilianza tangu mwaka 1939 zikasimama na baadaye mnamo miaka ya 1950 shughuli hizo zikaendelea tena na kusimama. Ilipofika mwaka 1986 Rais Museveni aliita timu ya Wataalam ili kuweka mikakati  ya namna ya kuendeleza shughuli za  utafiti wa mafuta na ilipotimu mwaka 1993 aliteua wataalam ambao walipatiwa mafunzo na hatimaye wakafanikisha ugunduzi wa mafuta hayo.

Mradi huo unaojulikana kama Mradi wa Bomba la Mafuta  la Afrika Mashariki (EACOP) utakuwa  na urefu wa kilomita 1145,  uwezo wa kusafirisha mapipa  216 ,000 kwa siku. Nchini Tanzania bomba litapita katika Mikoa 8, Wilaya 24,  vijiji 134 na Uganda Mikoa 8 na Wilaya 24.

[caption id="attachment_22386" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni (mwenye shati nyeupe) akiteta jambo na Mshauri Mkuu wa Rais wa Mafuta na Gesi wa Uganda Dkt. Kabagaambe Kalisa. Wanaofuatilia ni Waziri wa Viwanda wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, Waziri Ofisi ya Rais Zanzibar, Omar Haji, Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Grace Mgovano na Katibu Mkuu wa Nishati Dkt. Hamis Mwinyimvua.[/caption] [caption id="attachment_22387" align="aligncenter" width="750"] Wawakilishi wa Kampuni za Mafuta za TULLOW, TOTAL na CNOOC watakaojenga bomba.[/caption]

Bomba la EACOP litajengwa na kuendeshwa na Kampuni ya Bomba la Mafuta kwa ubia na Kampuni ya Taifa ya Mafuta ya Uganda (NOC), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Kampuni za Mafuta za  TOTAL ya Ufaransa, TULLOW ya Ireland  na CNOOC ya China.

Kutokana na asili ya mafuta ghafi ya Uganda  kuwa na nta na yenye mnato, bomba litahitaji kuwa na joto kwenye njia nzima nakufanya bomba la EACOP kuwa refu kuliko yote duniani lenye mfumo wa joto.

Njia ya Tanzania ilichaguliwa na Serikali ya Uganda kutokana na kuwa ya gharama nafuu na yenye uimara.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi