Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Mstaafu Dkt. Kikwete Akutana na Katibu Mkuu Afya
Oct 18, 2023
Rais Mstaafu Dkt. Kikwete Akutana na Katibu Mkuu Afya
Muasisi na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF), Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. John Jingu na ujumbe wake alipokutana nao ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo Jumatano tarehe 18 Oktoba, 2023.
Na Mwandishi Wetu

Muasisi na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF), Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amefanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. John Jingu na ujumbe wake alipokutana nao ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo Jumatano tarehe 18 Oktoba 2023. 

 

Pamoja na mambo mengine, mazungumzo yao yalihusu zaidi maandalizi ya Mkutano wa Pili wa Kisayansi wa Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto, Kijana, na Lishe (RMNCAH+N) uliopangwa kufanyika tarehe 15-17 Novemba 2023.

 

Mkutano huo, unaoandaliwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na washirika kadhaa ikiwa ni pamoja na JMKF, umepangwa kufanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam chini ya kauli mbiu: "Kukuza upatikanaji wa Huduma Bora za Uzazi, Mama na Mtoto, Kijana".

Makundi mbalimbali ya wajumbe wa ndani na wa kimataifa wanatarajiwa kuhudhuria Mkutano huo ambao ulitokana na mikutano ya awali ya wadau wa RMNCAH. 

 

Wazo la kufanyika kwa mkutano huo wa kila mwaka lilizaliwa katika moja ya mikutano ya kawaida ya kila robo ya Kikundi cha Kazi cha Kiufundi cha RMNCAH kwa lengo la kuleta wadau muhimu pamoja ili kusambaza, kuthibitisha, na kujifunza mafundisho yanayopatikana kwa vitendo bora na hatua za msingi zinazotokana na ushahidi ili kuzidisha utekelezaji.

Wizara ya Afya na washirika waliandaa mkutano wa kwanza wa RMNCAH mwezi Novemba, 2021 katika ukumbi huo uliofunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa ambapo zaidi ya wajumbe 1,400, wakiwemo wataalamu wa ndani na wa kimataifa walihudhuria.

 

Katika Mkutano wa Mwaka 2021, majadiliano makubwa yalitokana na mazungumzo katika vikao vidogo vidogo vilivyohusisha zaidi ya mawasilisho 200 yaliyolenga kuboresha mazingira wezeshi pamoja na upatikanaji wa huduma bora za RMNCAH + N nchini Tanzania.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi