Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan Ashiriki Maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru 2022
Oct 14, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Kagera katika Maadhimisho ya Kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru ambayo yamefanyika kwenye uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera tarehe 14 Oktoba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa vyeti kwa wakimbiza mwenge Kitaifa katika kilele cha mbio za Mwenge mkoani Kagera tarehe 14 Oktoba, 2022.
Vijana wa Halaiki wakitumbuiza kwa kuonesha kazi mbalimbali katika Kilele cha Maadhimisho ya Mbio za Mwenge wa Uhuru ambayo yamefanyika kwenye uwanja wa Kaitaba, Bukoba Mkoani Kagera tarehe 14 Oktoba, 2022.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera kwenye Maadhimisho ya Kilele cha Maadhimisho ya mbio za Mwenge wa Uhuru ambayo yamefanyika kwenye uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani humo leo tarehe 14 Oktoba, 2022.