Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan Apokea Ripoti ya Kikosi Kazi Kuhusu Uratibu Maoni ya Wadau wa Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa
Oct 21, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali pamoja na Wajumbe wa Kikosi Kazi Kuhusu Uratibu Maoni ya Wadau wa Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 21 Oktoba, 2022.
Viongozi pamoja na Wajumbe wa Kikosi Kazi kuhusu Uratibu Maoni ya Wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa wakisikiliza hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 21 Oktoba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Mwenyekiti wa Kikosi Kazi kuhusu Uratibu Maoni ya Wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa, Profesa Rwekaza Mukandala pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Kikosi Kazi hicho, Hamad Rashid Mohamed mara baada ya kupokea Ripoti ya Kikosi Kazi hicho Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 21 Oktoba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Kikosi Kazi kuhusu Uratibu Maoni ya Wadau wa Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa, Profesa Rwekaza Mukandala, Makamu Mwenyekiti Hamad Rashid Mohamed pamoja na Wajumbe wa Kikosi Kazi hicho mara baada ya kupokea Ripoti yao Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 21 Oktoba, 2022.