Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan Aanza Ziara Rasmi ya Kiserikali, Maputo Nchini Msumbiji
Sep 21, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi wakati akikagua Gwaride la Heshima mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Maputo leo tarehe 21 Septemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi wakati wakiangalia Gwaride la Heshima likitoka kwenye Viwanja vya Ikulu ya Maputo nchini humo tarehe 21 Septemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi kabla ya kuanza mazungumzo yao yaliyofanyika kwenye Ikulu ya Maputo leo tarehe 21 Septemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi katika Ikulu ya Maputo leo tarehe 21 Septemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi wakati walipokuwa wakizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Ziara yake Rasmi ya Kiserikali nchini humo.