Rais Mhe. Samia Azungumza na Watanzania Wanaoishi Nchini Ufaransa
Feb 14, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mhe. Liberata Mulamula, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Samwel Shelukindo pamoja na Watanzania waishio Ufaransa wakiimba wimbo wa Taifa mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Ubalozi, Paris nchini Ufaransa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Watanzania wanaoishi nchini Ufaransa katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania Jijini Paris jana tarehe 13 Februari, 2022.
Watanzania Waishio nchini Ufaransa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati akizungumza nao katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania Jijini Paris jana tarehe 13 Februari, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Watoto Watanzania ambao Wazazi wao wanaishi nchini Ufaransa jana tarehe 13 Februari, 2022
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Watanzania waishio nchini Ufaransa baada ya kuwasikiliza na kuzungumza nao katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania Jijini Paris jana tarehe 13 Februari, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Watanzania wanaoishi nchini Ufaransa mara baada ya kuzungumza nao jana Paris nchini Ufaransa.