Rais Mhe. Samia Awasili Nchini Mara Baada ya Kuhitimisha Ziara Yake ya Kikazi Nchini Ufaransa na Ubelgiji
Feb 20, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam waliofika kumpokea wakati akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 20 Februari, 2022 mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi katika nchi ya Ufaransa na Ubelgiji.
Sehemu ya Wananchi wakishangilia mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 20 Februari, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam waliofika kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 20 Februari, 2022 mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi katika nchi ya Ufaransa na Ubelgiji.