Rais Mhe. Samia Ashiriki Mkutano wa 22 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha
Jul 21, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na baadhi ya Viongozi Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na Wawakilishi wakati wa Wimbo wa Taifa wa Afrika Mashariki ukipigwa kwenye ukumbi wa Mikutano wa AICC Jijini Arusha kabla ya kuanza kwa Kikao cha Wakuu hao wa Nchi tarehe 21 Julai, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais wa Burundi, Mhe. Évariste Ndayishimiye mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha AICC kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 22 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ulionza tarehe 21 Julai, 2022 Jijini Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika Mkutano wa 22 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ulionza tarehe 21 Julai, 2022 Jijini Arusha