Rais Mhe. Samia Apokea Ripoti ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020
Aug 23, 2021
Na
Jacquiline Mrisho
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (NEC), Mhe. Jaji Rufaa (Mst) Semistocles Kaijage,akiwasilisha Ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania uliofanyika Mwaka 2020, wakati wa hafla ya kukabidhi ripoti hiyo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan(kushoto) na (kulia) Makamu wa Rais wa Tanzania, Mhe.Dkt.Philip Isdor Mpango na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, wakifuatilia ripoti hiyo, ikiwasilishwa katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu Jijini Dar es Saaam.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akifuatilia hutuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan.(hayupo pichani) akizungumza baada ya kukabidhiwa kwa Ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania kwa mwaka 2020, na(kushoto kwake) Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Dkt.Philip Isdor Mpango na (kulia kwake) Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson Pamoja na Mabalozi mbalimbali mara baada ya hafla ya upokeaji wa Ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020.