Rais Mhe. Samia Afungua Rasmi Daraja la Tanzanite na Barabara Unganishi Jijini Dar es Salaam
Mar 24, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe. Samia Suluhu Hassan akiondoa kitambaa pamoja na Balozi wa Korea hapa nchini, Kim Sun Pyo kuashiria ufunguzi rasmi wa Daraja la Tanzanite lenye urefu wa Kilometa 1.03 pamoja na Barabara zake unganishi zenye urefu wa Kilometa 5.2 kuanzia eneo la Agha Khan (Barack Obama Road) hadi eneo la Coco Beach Jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi. Rogatus Mativila pamoja na viongozi wengine wa Serikali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria ufunguzi Rasmi wa Daraja la Tanzanite lenye urefu wa Kilometa 1.03 pamoja na Barabara zake unganishi zenye urefu wa Kilometa 5.2 kuanzia eneo la Agha Khan (Barack Obama Road) hadi eneo la Coco Beach Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa wakitembelea na kukagua Daraja la Tanzanite lenye urefu wa Kilometa 1.03 pamoja na Barabara unganishi zenye urefu wa Kilometa 5.2 kuanzia eneo la Agha Khan (Barack Obama Road) hadi eneo la Coco Beach Jijini Dar es Salaam mara baada ya kulizindua rasmi leo tarehe 24 Machi 2022.