Rais Mhe. Samia Aanza ziara ya Siku Moja Nchini Congo
Aug 18, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo akikagua Gwaride rasmi alipowasili katika Viwanja vya Ikulu Jijini Kinshasa kwa ajili ya kuanza ziara rasmi ya siku moja nchini DRC tarehe 18 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo alipokua akitambulishwa kwa Viongozi mbalimbali wa DRC alipowasili katika Ikulu ya Kinshasa kwa ajili ya kuanza ziara rasmi ya siku moja tarehe 18 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo katika Ikulu ya Kinshasa nchini DRC tarehe 18 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo alipowasili katika Viwanja vya Ikulu ya Kinshasa tarehe 18 Agosti,2022.