Rais Mhe. Samia Aanza Ziara Mkoani Mbeya kwa Kuzungumza na Wananchi na Kuzindua Miradi ya Maendeleo
Aug 05, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali wakati akizindua Mradi wa Maji safi wa Mbalizi, Shongo-Igale katika eneo la Mbalizi mkoani Mbeya leo tarehe 05 Agosti, 2022. Wengine katika picha ni Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akifungulia maji kuashiria uzinduzi wa mradi wa maji safi wa Shongo-Mbalizi katika eneo la Mbalizi mkoani Mbeya leo tarehe 05 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Mbalizi mkoani Mbeya mara baada ya kuzindua mradi wa maji safi wa Shongo-Mbalizi tarehe 05 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi pamoja na Wafanyakazi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya Kitengo cha Wazazi na Watoto Wachanga META mara baada ya kuzindua ujenzi wa jengo la afya ya huduma ya mama na mtoto META mkoani Mbeya tarehe 05 Agosti, 2022.
Jengo la afya ya Huduma ya Mama na Mtoto lililopo Meta Mkoani Mbeya ambalo limewekewa jiwe la Msingi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 05 Agosti, 2022. tarehe 05 Agosti, 2022.