Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Magufuli Kufungua Maonesho ya Biashara Sabasaba
Jun 27, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_4504" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akizungumza katika moja ya matuki ya wizara hiyo.(Picha ya Maktaba)[/caption]

Na: Mwandishi Wetu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, anatarajiwa kufungua Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu kama Sababsaba Julai Mosi mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa kwa Vyombo vya Habari iliyotolewa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, Rais atafanya ufunguzi huo katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Slaam.

Waziri Mwijage ameeleza katika taarifa hiyo kuwa lengo la maonesho ni kutoa fursa kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi, pamoja na taasisi mbalimbali kutangaza biashara na huduma, kutoa fursa kwa wafanyabisashara wa ndani kujifunza mambo ya biashara na uzalishaji bora wa bidhaa kulingana na soko la kimataifa, kutengeneza mitandao ya mawasiliano baina yao ambayo itasaidia kukuza biashara na kufikia malengo waliyojiwekeka na pia kutoa fursa ya kuuza bidhaa.

“Maonesho haya yanabeba kauli mbiu isemayo Ukuzaji wa Biasha kwa Maendeleo ya Viwanda, inanalenga kutumia Maonesho haya kama jukwaa la kutangaza biashara na huduma mbalimbali kwa ajili ya ukuzaji wa sekta ya viwanda, ikizingatiwa kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inaweka mkazo mkubwa katika kuendeleza uchumi wa viwada hapa nchini”, anaeleza taarifa ya Waziri.

Aidha Maonesho ya mwaka huu yatatoa fursa kwa wenye viwanda vidogo, vya kati na vikubwa kukutana na wanunuzi wa bidhaa zao na kutakuwa na kampeni maalum ya kuhamasisha wananchi kupenda na kutumia bidhaa zinazozalishwa hapa nchini

“Napenda kuwafahamisha kuwa Tan Trade kwa kushirikiana na washirika wake kwa mara ya kwanza imeandaa Siku ya ‘Afrika Mashariki’ ambayo itaadhimishwa tarehe 6 Julai, 2017. Lengo la siku hii ni kuimarisha biashara katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kama inavyojulikana nchi hizi zimejaliwa kuwa na rasilimali nyingi hali ambayo itatoa fursa nzuri katika maendeleo ya kiuchumi katika nchi hizo ili kuwe na uchumi endelevu”, ilieleza taarifa hiyo.

Katika maonesho hayo, Waziri anaeleza kuwa Tan Trade imeandaa eneo maalum litakalojulikana kwa jina la ‘Banda la Tanzania’ kwa ajili ya wazalishaji wa bidhaa mbalimbali zinazotengenzezwa ndani ya nchi na ‘Banda la Asali’ kwa ajili ya kukuza bidhaa za nyuki na pia kutakuwa na eneo maalum la wazalishaji wa bidhaa za ngozi ambalo washiriki wake watapata fursa ya kuonesha bidhaa bora za ngozi kwa ajili ya kuvutia wananchi wengi kupenda bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.

[caption id="attachment_4505" align="aligncenter" width="800"] Wananchi wakiwa katika foleni ya kuingia katika Viwanja vya Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa
vya Mwalimu J.K. Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam. [/caption]

Katika kuimarisha huhusiano wa kibishara na kuwakutanisha wafanyabiashara wa Kitanzania na wenzao kutoka nje ya nchi, kutakuwa na banda maalum kwa ajili ya mikutano ya kibiashara yaani Business to Business (B2B) na pia banda maalum litakalotumika kwa utoaji wa mafunzo ya kibiashara.

Hadi sasa washiriki zaidi ya 2500 kutoka ndani na nje ya Afrika wamethibitisha kushiriki Maonesho ya mwaka huu. Nchi zitakazoshiriki ni Burundi, China, Comoro, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Misri, Ujerumani, Ghana, India, Indonesia, Iran, Italia, Japan, Kenya, Malawi na Mauritius.

Nchi zingine ni pamoja na Morocco, Msumbiji, Namibia, Pakistani, Rwanda, Singapore, Afrika Kusini, Sudani Kusini, Syria, Uturuki, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Uganda, Marekani, Uingereza na Vietnam.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi