Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Magufuli Ayataka Mataifa ya Afrika Kujiepusha na Masalia ya Fikra za Kikoloni
Aug 29, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_46361" align="aligncenter" width="750"] Rais Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Mtendaji Mkuu wa
Taasisi ya Uongozi, Profesa Joseph Semboja, alipowasili kuhutubia
Mkutano wa sita Jukwaa la Uongozi Afrika katika Ukumbi wa Jakaya
Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 20, 2019[/caption] [caption id="attachment_46362" align="aligncenter" width="750"] Rais Dkt. John Pombe Magufuli akijiunga na viongozi
wastaafu kukiliza majadiliano wakati wa Mkutano wa Sita Jukwaa la
Uongozi la Afrika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es
salaam leo Agosti 20, 2019[/caption]

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa wito kwa Mataifa ya Afrika kutafsiri vizuri dhana ya uhuru na kujiepusha na masalia ya fikra za kikoloni za kuamini kuwa watawala wa zamani wa Mataifa ya Afrika ndio wenye uwezo wa kusaidia kusimamia na kuendeleza rasilimali zilipo katika Bara la Afrika.

Mhe. Rais Magufuli ametoa wito huo leo tarehe 29 Agosti, 2019 Ikulu Jijini Dar es Salaam alipohutubia Mkutano wa 6 wa Jukwaa la Uongozi Afrika unaohudhuriwa na Marais Wastaafu Mhe. Benjamin William Mkapa (Tanzania), Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (Tanzania), Mhe. Thabo Mbeki (Afrika Kusini), Mhe. Hassan Mohamud (Somalia), Mhe. Hery Rajaonarimampianina (Madagascar), Mabalozi, Wawakilishi wa Kimataifa na washiriki wa Jukwaa la Uongozi Afrika.

Mhe. Rais Magufuli amefafanua kuwa dhana ya uhuru haiwezi kutenganishwa na kujitegemea kwani bila kujitegemea uhuru wa Taifa husika utakuwa mikononi mwa linayemtegemea.

“Maana hasa ya kupigania uhuru ilikuwa ni kurejesha rasilimali na hasa maliasili zetu lakini pia kuwa na maamuzi kamili kuhusu namna ya kuzisimamia na kuzitumia kwa manufaa yetu ili kuleta ukombozi wa kiuchumi, na hii ndio maana pekee ya kulinda uhuru wa kisiasa.

Tusijidanganye watawala wetu wa zamani hawawezi kugeuka kwa usiku mmoja na kuwa wajomba zetu au wakombozi wetu kiuchumi, utegemezi huu ndio umeimarisha mizizi na misingi ya ukoloni mamboleo, ni lazima tuamke” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

[caption id="attachment_46363" align="aligncenter" width="750"] John Pombe Magufuli akihutubia Mkutano wa Sita
Jukwaa la Uongozi la Afrika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu
jijini Dar es salaam leo Agosti 20, 2019[/caption]

Ametaja sababu ya 2 inayosababisha usimamizi mbaya wa rasilimali za Bara la Afrika kuwa ni tafsiri potofu ya msingi wa maendeleo kwa kudhani fedha ni msingi wa maendeleo hali iliyosababisha viongozi wake kuzunguka katika Mataifa tajiri kuomba misaada na mikopo ambayo inawezekana inatokana na rasilimali za Afrika, badala ya kuelekeza nguvu katika kusimamia na kutumia rasilimali zilizopo huku akisisitiza maneno ya Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliyesema ili tuendelee tunahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora.

Sababu nyingine ni ukosefu wa ubunifu na teknolojia ya viwanda ambavyo vitaongeza thamani ya bidhaa za Afrika na kuzalisha ajira, migogoro na hali tete ya kisiasa inayosababishwa na mabeberu wanaotaka kuendelea kutumia maliasili za Afrika kwa manufaa yao, watendaji na viongozi wa Afrika kuingia mikataba mibovu na wawekezaji bila kujali maslahi ya Afrika kutokana na kukosekana kwa uzalendo na uharibifu wa maliasili unaosababishwa na uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi.

[caption id="attachment_46364" align="aligncenter" width="750"] Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Rais Mstaafu wa Awamu ya
Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa na Rais Mstaafu wa Nigeria Jenerali
Olusegun baada ya kuhutubia Mkutano wa Sita Jukwaa la Uongozi Afrika
katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti
20, 2019[/caption]

Mhe. Rais Magufuli amelipongeza Jukwaa la Uongozi Afrika kwa kuja na kauli mbiu isemayo “Kuimarisha Usimamizi Bora wa Maliasili kwa ajili ya Mageuzi ya Kijamii na Kiuchumi Afrika” na kubainisha kuwa kauli mbinu hiyo inaonesha umuhimu wa kujenga mifumo mipya ya kusimamia na kutumia rasilimali kwa manufaa ya watu wake.

Ametaja baadhi ya hatua zilizoanza kuchukuliwa na Tanzania katika kusimamia matumizi bora ya maliasili ili kufikia mageuzi ya kijani na kiuchumi kuwa ni kutunga sheria ya kulinda utajiri na rasilimali za Tanzania ya mwaka 2017, kupitia upya na kurekebisha mikataba ya uchimbaji wa madini isiyokuwa na manufaa kwa Taifa, kuweka msukumo mkubwa katika ujenzi wa viwanda na ukuzaji wa teknolojia ya viwanda na kudhibiti uharibifu wa maliasili za misitu na kulinda baionowai.

Hatua nyingine ni kutekeleza miradi mikubwa ya kuzalisha nishati ya umeme ukiwemo mradi mkubwa wa kujenga Bwawa la Nyerere katika mto Rufiji utakaozalisha megawati 2,115 za umeme, kuongeza maeneo ya uhifadhi kwa kuongeza Hifadhi za Taifa 3 mpya, kudhibiti nidhamu ya watumishi wa umma, kudhibiti ufisadi na ubadhirifu na kwamba matokeo ya hatua hizo yameanza kuonekana.

[caption id="attachment_46365" align="aligncenter" width="750"] Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu
Hassan na viongozi wastaafu katika picha ya pamoja na Sekretarieti ya
Taasisi ya Uongozi baada ya kuhutubia Mkutano wa Sita Jukwaa la
Uongozi Afrika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es
salaam leo Agosti 20, 2019[/caption] [caption id="attachment_46366" align="aligncenter" width="750"] Rais Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia Mkutano wa Sita
Jukwaa la Uongozi la Afrika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu
jijini Dar es salaam leo Agosti 20, 2019[/caption]

Washiriki wa mkutano huo unaofanyika kwa siku 2 wakiwemo Marais Wastaafu wameeleza umuhimu wa viongozi wa Afrika kutoa kipaumbele katika masuala muhimu yanayowahusu na kwa kushirikiana na kubadili mtazamo na fikra za utegemezi.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

29 Agosti, 2019

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi